Uongozi wa Klabu ya Geita Gold FC umezindua kadi mpya ya wanachama inayofahamika kwa Jina la MID- ELECTRONIC CARD kwa lengo la kusaidia Klabu hiyo kujiingizia Mapato.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Simon Shija amesema lengo lao ni kusaidia timu hiyo ambayo imekuwa na changamoto za kifedha hali ambayo imepelekea kuzindua mfumo huo kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.

Shija amesema Mwanachama atawajibika kuchukua kadi hiyo kwa kulipia kiasi cha Shilingi 36000 kwa mwaka huku kwa mwezi ikiwa ni shilingi Elfu 3 na kusema fedha hizo zitalipwa kupitia namba za mawakala.

“Kwa sasa hivi tuna bilioni 1.6 kwa mwezi mwanachama atalipia shilingi elfu 3 lakini tunapendelea kabisa mwanachama anayependa klabu yake ili uweze kuendesha vizuri inabidi ulipie shilingi elfu 36 uwe na uwezo wa kupata kadi lakini uweze kuisaidia klabu yako kuweza kuendesha shughuli zake za kila siku, ” amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu Geita Gold.

Geita Gold inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu watatu mfululizo, baada ya kupanda Ligi Kuu msimu wa 2020/21 ikitokea Ligi Daraja la Kwanza (Championship).

Ni moja ya klabu za Ligi Kuu ambazo zinamiliki Uwanja wake, ambao utaanza kutumika rasmi msimu wa 2023/24, na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji elfu kumi na mbili (12.000).

Mabingwa CECAFA wapongezwa Dodoma
Mohamed Elneny aongezewa mmoja Arsenal