Msafara wa Viongozi na Wachezaji wa Fountain Gate School Jana Jumanne (Februari 21), ulilazimika kusimama maeneo kadhaa kabla ya kurejea Kambini kwao na kupokelewa Kifalme baada ya kutwaa ubingwa wa African Schools Championship Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’.

Msafara huo ulitua Morogoro kupata kifungua kinywa, na baadae Gairo kupata chakula cha Mchana, kabla ya kutua viunga vya Dodoma ambako walipokelewa Kifalme na Viongozi mbalimbali, Wananchi na Wafanyakazi wa taasisi hiyo ambao kwa pamoja waliwapongeza Wachezaji hao kwa kupambana mpaka kupata ubingwa huo na kuisaidia taasisi yao kuvuna zaidi ya Shilingi Million 200 za Kitanzania.

Mapokezi hayo na pongezi hizo kwa Viongozi na Wachezaji zinaongeza morali kwa kiasi kikubwa kuelekea kwenye mashindano ya African Schools Championship ya Bara la Afrika, ambayo yanatarajia kutimua vumbi Nchini Afrika Kusini Mwezi Aprili mwaka huu.

Historia: Biblia kongwe Duniani kuuzwa kwa mnada
Wanachama Geita Gold kumiliki KADI