Jumla ya Wanajeshi 11 wa Somalia, wameuawa hii leo katika shambulizi lililofanywa kwenye kambi yao kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu, huku kundi la al-Shabaab likidai kuhusika na shambulio hilo.

Kamanda wa kundi la wanamgambo wenye mafungamano na Serikali ya mjini Mogadishu, Mohamed Osman amesema Afisa mmoja wa cheo cha juu ni miongoni mwa wahanga wa shambulizi hilo, na kuongeza wanamgambo wa al-Shabaab pia waliuawa.

Wanajeshi wakitazama uharibifu wa bomu katika moja ya barabara za nchini Somalia. Picha ya The New York Times.

Osman amesema, al-Shabaab imelipua gari lililojaa viripuzi kwenye kambi hiyo na kisha wapiganaji wake wakafanya uvamizi huku Kamanda wa jeshi la Somalia katika mji wa Balcad ulio karibu na kambi iliyoshambuliwa akisema serikali inalidhibiti eneo hilo.

Shambulizi hilo la al-Shabaab, limefanyika ikiwa ni siku moja baada ya Serikali kuukomboa mji muhimu wa mwambao wa Haradhere kutoka mikononi mwa kundi hilo.

Mtoto wa Rais akamatwa kwa amri ya kaka yake
Bondia Mandonga akabidhiwa gari