Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imeliomba Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kutoijibu barua waliyopewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuitaka Serikali kuwaomba radhi waumini wa dhehebu hilo.

Kauli hiyo imetolewa kwa niaba ya Upinzani bungeni Jijini Dodoma na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia ambapo amesema kuwa Waziri Mkuu ndiyo msimamizi na mdhibiti wa shughuli za Serikali bungeni na swali lililoulizwa leo lilitaka kupata majibu kuhusu hatima ya KKKT.

Wamesema kuwa kuanzia sasa watahakikisha wanatumia mbinu mbalimbali ndani ya Bunge kuitaka Serikali kutoa majibu ya kina kuhusu barua hiyo.

“Wasiwajibu Serikali halafu waone Serikali itachukua hatua gani kwani nchi hii si mali ya Serikali. Waumini wako katika hamaki, viongozi hawa wa dini ni Watanzania na wana haki ya kutoa maoni, Serikali inapaswa kuwaomba radhi waumini,”amesema Mbatia

Hata hivyo, Serikali imetoa siku 10 kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kufuta waraka wake wa Pasaka uliotolewa Machi 24, 2018.

 

Foleni ya Tazara mwisho Septemba
Kala Jeremiah akumbuka alivyolazimishwa kuimba kama ‘Kingwendu’