Waziri wa michezo nchini Tanzania, Dkt. Harrison Mwakyembe amewatakia safari njema watoto waliochaguliwa na kampuni ya Tecno mobile kwenda kufanya majaribio ya kucheza mpira wa miguu katika Academy ya klabu ya Manchester City nchini Uingereza.

Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa serikali ina furaha kuona wadau wanajitokeza kukuza vipaji nchini Tanzania, hasa kwa wadodo wanaochipukia.

“Niwaombe wadau katika sekta ya michezo tushirikiane katika kukuza michezo, nawashukuru kampuni ya Tecno Mobile kwa kuonesha juhudi za wazi katika kufanikisha hili, Serikali pia inafanya jitihada kwa nafasi kuhakikisha viwango vya soka na michezo kwa ujumla vinakua.” ameongeza Dkt. Mwakyembe.

Akiongea katika hafla hiyo fupi kutambulisha mbele ya waziri mpango huo, Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Tecno Mobile, Eric Mkomoya amesema kuwa kampuni ya Tecno Mobile ndio wadhamini pekee wa safari hiyo kupitia simu yao mpya Tecno Camon Cx toleo maalumu la machester city ambapo watoto hao wawili wataenda kupewa mafunzo yenye kiwango cha kimataifa lakin pia endapo watafanya vizuri wanaweza kuchaguliwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo.

“Tumefurahi kukutana na serikali hasa Waziri wa michezo na kuamua kuwapa Baraka zake vijana wetu wanaokwenda huko wataondoka usiku wa tarhe 23 na kurudi tarehe 30 mwezi wa nane”  amesema Mkomoya

Nao wazazi wameeleza kufaha yao kuona vijana wao amepata nafasi hiyo kwani wanaamini kuwa watoto wao watafanya vizuri katika fursa hiyo.

Watoto wawilli Daudi Damasi pamoja na Malimi Majaliwa wenye umri wa miaka 12, wanaocheza nafasi ya kipa na ushambuliaji wamepata nafasi hizo kutokana na ushirikiano wa Tecno Mobile na asasi ya michezo ya Magnet, na wataondoka kuelekea manchster city mnamo tarehe 23 mwezi wa nane na kurudi nchini tarehe 30.

Msafara huo utaongozwa na wazazi na walezi watoto hao akiwemo kocha mwenye utalaamu wa kulea vipaji vya vijana kocha Juma Maswanya.

Tecno mobile ndio wadhamini wakuu wa safari hiyo ambapo wanajumuisha vijana kutoka nchi za afrika ambazo ni Nigeria, Misri , Tanzania, Ghana pamoja na Kenya.

 

Timu Sita Kupanda Ligi Kuu Msimu Wa 2018/19
Video: Manji anatumia 'unga' - Mkemia Mkuu, Bombardier yamtia Lissu matatani