Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Watanzania wanapaswa kujifunza namna ya kuishi na ugonjwa wa corona kwa sababu utaendelea kuwepo kwa miezi kadhaa.

Ameeleza kuwa maisha na shughuli za kila siku zinatakiwa kuendelea kama kilimo, uvuvi na biashara licha ya uwepo wa virusi hivyo. Hivyo, amewataka wananchi kujifunza zaidi namna ya kuvikabili.

“Corona itaendelea kuwepo kwa miezi kadhaa ni lazima tujifunze kuishi na corona ni lazima maisha yaendelee kilimo kiendelee, uvuvi uendelee, biashara ziendelee, uzalishaji mali uendelee muhimu ni kuchukua tahadhari,” amesema.

Ameyasema hayo wakati wa kutoa mafunzo kwa watoa huduma wa ngazi ya jamii katika kufanya ufatiliaji wa tetesi za wagonjwa wa Covid-19 na watu wanaokaa karibu na wagonjwa, mkakati uliohusisha Hospitali ya Benjamin Mkapa na shirika la Afya Duniani (WHO).

Mahakama ya Rufani yawaachia huru waliofungwa miaka 20 kwa ujangili
Polisi Tabora yaonya wanafunzi kushiriki kwenye wizi