Jeshi la polisi Mkoani Tabora limesema litawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wakiwemo watoto washule watakao bainika kujihusisha na vitendo vya kihalifu au wizi wa mali za wananchi.

Hayo yamesema na Kamanda wa Polisi Mkoani humo ACP Barnabas Mwakalukwa alipokuwa akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watu 20 waliojihusisha na wizi wamali za wananchi.

Amesema miononi mwa vijana waliokamatwa wamo watoto wadogo wenye umri wa chiniya miaka 18 ambao pasiposhaka bado ni wanafunzi na kwa kipindi hiki wapo kwenye mapumziko baada ya kufungwa shule na vyuo kutokana na uwepo wa ugonjwa wa Covid 19.

”Natoa onyo kwa watoto wote wasiotulia nyumbani na kuanza kujiingiza katika matukio ya wizi, tutawakamata wahalifu wote na kuwafikisha mahakamani pasipo kujali kama kuna mwananfunzi au la, mahakama itajua nini cha kufanya” ameeleza kamanda Mwakalukwa

Serikali: Watanzania tujifunze kuishi na corona
Kupambana na corona: Ndege ya WFP kutua Dar leo na wafanyakazi