Watu watano wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo Novemba 21,2020, baada ya magari mawili ya mizigo kugongana uso kwa uso na kuwaka moto eneo la Kitumbi, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Ajali hiyo imehusisha magari aina ya Kenta na Lori, ambapo chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni uzembe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Blasius Chatanda, amesema gari aina ya Toyota Kenta lilikuwa linatokea Dar es Salaam kwenda Lushoto na Lori lilikuwa linatoka Tanga kwenda Dodoma.

Majeruhi amelazwa katika kituo cha afya cha Mkata anaendelea na matibabu.

Trump kushiriki mkutano wa G20
Sekondari ya Ukwamani yapokea mchango wa komputa

Comments

comments