Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amepiga marufuku jeshi la polisi kukamata wafanyabiashara ya mahindi wakati wanapopeleka bidhaa yao sokoni kwani hali hiyo inakatisha tamaa wakulima ambao hupambana kujikwamua na umaskini na kuchangia pato la taifa. .

Waziri Mkenda ametoa Kauli  hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mashamba ya kilimo cha mkataba wa zao la mtama wilayani Kongwa.

Amesema kuwa anatarajia kuzungumza na Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini (IGP) kuhakikisha jeshi hilo linaachana na tabia ya kukimbizana na wafanyabiashara hao wakati wakipeleka biashara zao sokoni.

“Hiki kitu kwa kweli sio kizuri hawa ni watanzania ambao wanatafuta masoko ya zao hilo ni vema wakaachiwa ili kuendelea na biashara hiyo,” amesema Prof. Mkenda

Sambamba na hayo Waziri Mkenda amewataka maafisa ugani kuendelea kutoa elimu kwa wakulima wa mazao mbalimbali wilayani humo ili wafanye kilimo chenye tija ambacho kitaleta matokeo chanya kwao na taifa kwa ujumla.

Serikali kutekeleza uwekezaji mto msimbazi
Rushwa ya Mil. 100 yawaponza askari