Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Japan, Shinzo Abe ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi Julai 8, 2022 umezikwa hii leo jijini Tokyo.

Katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Tokyo maelfu ya wananchi walikusanyika ili kutoa salamu zao za mwisho kwa Hayati Abe, baada ya Mamlaka kuupitishwa mwili huo ukiwa kwenye gari maalum wakati ukipelekwa eneo la Zojoji.

Katika eneo hilo, wageni mbalimbali, ndugu na viongozi mbalimbali, pia walipata nafasi ya kutoa salamu zao za katika Jeneza la Abe.

Ukali wa maisha: Waganda waandamana, wakamatwa na Polisi
Wanajeshi 50 wakamatwa nchini Mali, wadaiwa ni mamluki