Mamlaka za usalama nchini Mali, zimewakamata wanajeshi 50 wa Ivory Coast waliokuwepo nchini humo wakifanya kazi katika kampuni ya kandarasi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa.

Hatua hiyo, inatokana na tuhuma za Serikali ya Mali inayodai wanajeshi hao wa Ivory Coast ni mamluki, hatua ambayo inaweza kuibua mvutano kati ya nchi hizo mbili za Afrika Magharibi.

Msemaji wa serikali ya Mali, Kanali Abdoulaye Maigadege amesema ndege mbili ziliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mali Julai 10, 2022 zikiwa na wanajeshi 49 “wakiwa na silaha zao na risasi za vita, pamoja na vifaa vingine vya kijeshi.

“Walikuwa wapo nchini kinyume cha sheria za eneo la kitaifa la Mali na serikali ya mpito inawachukulia kama mamluki, hivyo tunawashikilia,” amesema Maigadege.

Naye Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, Olivier Salgado amesema wanajeshi hao wa Ivory Coast si sehemu ya mojawapo ya kikosi cha MINUSMA, lakini wapo kwa miaka kadhaa nchini Mali kama sehemu ya usaidizi wa vifaa kwa niaba ya mmoja wa kikosi chao.

Alisema, taarifa za kuwasili kwao kwa ajili ya kutoa msaada katika eneo hilo, zingewasilishwa mapema kwa mamlaka ya kitaifa.

“Wanafanya kazi katika kampuni ya Ujerumani ambayo imepewa kandarasi na ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaojulikana kama Sahelian Aviation Services,” amefafanua Salgado.

Hata hivyo, Maigadege amebainisha kuwa watakomesha shughuli za ulinzi wa Huduma za Usafiri wa Anga za Sahelian na vikosi vya kigeni na kuwataka kuondoka katika ardhi ya Mali.

“Serikali imeialika kampuni ya anga ya ‘Sahelian Aviation Services kukabidhi usalama wake kwa vikosi vya ulinzi na usalama vya Mali,” alisema Maigadege.

Serikali ya mpito ya Mali, ilithibitisha mwezi Juni kwamba haitaidhinisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini Mali, huku Serikali ya nchi ya Ufaransa pia ikiondoa vikosi vyake.

Waziri Mkuu aliyeuawa azikwa kwa heshima
Dkt. Biteko: Rasilimali madini kuzidi kutanua uchumi wa taifa