Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Jumanne Shauri leo, Julai 11, 2022.

Majaliwa ametoa agizo hilo alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam na wa Halmashauri ya Ilala katika ziara yake aliyoifanya jijini Dar es Salaam.

Kusimamishwa kwa Shauri pamoja na watumishi wengine 9 wa Halmashauri hiyo kunakuja ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za serikali sh. Bilioni 10 ambazo zilikusanywa na hazikufikishwa benki kama ilivyotakiwa.

Taarifa inasema agizo hilo linatokana na matokeo ya ukaguzi wa CAG kuhusu mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na 2020/2021.

Pamoja na kusimamishwa kwao, pia wamekabidhiwa kwa Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 12, 2022
Majaliwa aagiza fedha za ndani zitumike katika miradi