Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, amepiga marufuku uwekaji wa Alarm, Ving’ora na Sports light kwenye magari ya watu binafsi kwani vinasababisha taharuki kwa watumiaji wengine wa barabara kwa kuhisi kwamba kuna msafara wa kiongozi au mgonjwa.
Ametoa agizo hilo leo Agosti 5 ikiwa ni kipindi cha Mkutano wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC na kwamba kuanzia kesho Agosti 6 msako mkali utaanza kufanywa na kuwakamata watakaokaidi agizo hilo na ni marufuku ya kudumu.
”Marufuku hiyo inakwenda kwa watu wote wenye magari waliyoweka alarm, isipokuwa kwa magari maalumu kama polisi na Ambulance, msako mkali unaanza kesho yeyote atakayekamatwa na hizo taa iwe urembo lakini unasababishia watu taharuki na kupaki magari na kunyimwa haki ya kutumia barabara, watakamatwa na sitowaachia mpaka watakapokuja na mafundi wao waje kuwabadilishia kituoni.” amesema Kamanda Mambosasa.
Kwa upande mwingine jeshi la polisi limepiga marufuku kwa madereva bodaboda wote, kufika katikati ya mji kwa kipindi hiki chote cha ugeni na kushauriwa waendelee kufanya biashara zao pembezoni mwa mji.
-
Muhimbili yakanusha taarifa za uwepo wa mtu anayesadikiwa kuwa ni mchawi Wodini
-
SADC: Bashungwa awaonesha ‘fursa’ wadau wa sekta binafsi
-
SADC: Bashungwa awaonesha ‘fursa’ wadau wa sekta binafsi