Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya madini kuharakisha mchakato wa kutafuta ufumbuzi wa suala la Madini ya Lithium mapema iwezekanavyo ili kuweka wazi viwango vya uongezaji thamani kwa madini hayo kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo, wakati akifungua Kongamano la Wachimbaji  Madini na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) kwenye ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.

Amesema kuwa Serikali imeendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kurasimisha maeneo yenye milipuko ya madini ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023 zimetolewa jumla ya leseni 6,381, zikiwemo leseni 3,865 za uchimbaji mdogo wa madini (PML), leseni 1,649 za biashara ndogo ya madini (Brokers).

Serikali nchini, imeendelea kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini ambapo hadi sasa jumla ya viwanda vitatu vya kusafisha wa dhahabu (Gold Refineries) vimeanzishwa .Viwanda vyote kwa pamoja vinauwezo wa kusafisha dhahabu kilogramu 515 kwa siku.

Waziri Mkuu azindua huduma upandikizaji uloto
Simba SC kumaliza ligi haste haste