Mkenya, Eliud Wekesa, maarufu kama “Yesu wa Tongaren” amefikishwa mahakamani mjini Bungoma baada ya kujisalimisha kwa maofisa wa polisi kwa mahojiano alipotakiwa kufanya hivyo hatua inayokuja wakati serikali ikijiridhisha na wahubiri wenye msimamo na itikadi kali.
Wekesa amekuwa akijitangaza kuwa yeye ndiye Yesu ambapo pia ana malaika wake anaosema wanamsaidia katika kazi yake kama kristo mwana wa Mungu na akimiliki malaika wake sambamba na wanafunzi 12 kama ilivyokuwa katika Bibilia na wakati wa Yesu Kristo mwana wa Mungu.
Polisi walimtaka kiongozi huyo wa dhehebu la New Jerusalem kufika kituoni kwa mahojiano kuhusu mafundisho yake ya kidini yanayotiliwa shaka, na Yesu huyo alitii na kufika kwa wakati kama ilivyotakikana na chombo hicho cha usalama.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari vya ndani, Wekesa amesema kuwa yeye hanatia yoyote ambayo imesababisha kutakiwa kuhojiwa na polisi. Amesisitiza kwamba yeye anafanya kazi ya kueneza injili kwa viumbe waliopotea.