Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Young Africans wameshindwa kufurukuta mbele ya Singida Utd katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo jioni Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans ambao walitarajiwa kulipiza kisasi katika mchezo huo, kufuatia kufungwa na kuondolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho (ASFC) majuma mawili yaliyopita dhidi ya Singida Utd, wameambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Singida Utd walikua wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya pili kupitia kwa mshambuliaji kutoa DR Congo Kambale Salita Gentil bada ya kunganisha wavuni mpira wa krosi uliopigwa na mshambuliaji wa pembeni Kigi Makasi.

Young Africans walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 45, baada ya beki kutoka visiwani Zanzibar Abdallah Haji Shaibu (Ninja) kuumalizia kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajibu.

Matokeo hayo ya sare, yanaiwezesha Young Africans kufikisha alama 47 baada ya kucheza michezo 22, na kufanya wawe nyuma kwa alama tano dhidi ya mahasimu wao katika soka la bongo Simba SC, wenye alama 52 za michezo 22.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi kuu ya soka Tanzania bara iliyochezwa jioni ya leo.

Mbao FC 2- 1 Njombe Mji

Stand Utd 1-3 Majimaji

Tanzania Prisons 1-1 Kagera Sugar

Mwadui FC  2- 1 Lipuli FC

Pep Guardiola afunguliwa mashtaka ya kinidhamu UEFA
JPM afanya uteuzi