Kocha wa zamani wa Young Africans Mwinyi Zahera amesema mshambuliaji Heritier Makambo anatamani kurudi Tanzania na kuwatumika Wananchi, lakini mesisitiza hatahusika na mpango wa kumrudisha

Taarifa zinasema kuwa Zahera aliuambia uongozi wa Young Africans kuwa, anaweza kuwasaidia kumrejesha Makambo kutoka klabu ya Horoya Ac anayoitumikia kwa sasa.

Ikumbukwe Zahera ndiye aliyesimamia usajili wa Makambo alipotua Horoya AC, ambako alisaini mkataba wa miaka mitatu, amebaki na mkataba wa mwaka mmoja kunako klabu hiyo.

“Taarifa za mimi kutaka kumrudisha Makambo Young Africans hazina ukweli wowote kwa sababu mimi sio Wakala wake”

“Lakini nafahamu Makambo anatamani kurudi Young Africans, mwenyewe amesema, siku moja atarudi tena Tanzania kuitumikia Yanga,” alisema Zahera

Tetesi za Makambo kurudi Young Africans zimezidi kushika kasi huku mashabiki wakimtaka Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said kumrejesha mshambuliaji huyo aliyeifunga mabao 21 katika msimu wake mmoja na Young Africans.

Inaelezwa Horoya AC wako tayari kumuuza lakini wanataka dau lisilopungua dola 45,000.

Young Africans ilimuuza Makambo kwenda Horoya kwa dau la dola 80,000 akisaini mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wa Guinea.

Kibwana: Sijui lolote kuhusu Djuma
Mwanamke ajitosa urais TFF