Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mwenyekiti wa shina (Balozi) namba saba katika Kijiji cha Ilambilole Kata ya Kising’a iliyopo Jimbo la Isimani katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Chongolo ameongoza harambee hiyo wakati wa ziara katika ubalozi huo ambapo viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi walioambatana naye kwenye ziara hiyo walichangia vifaa vya ujenzi na fedha taslimu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.
Ameagiza ujenzi wa nyumba hiyo uanze haraka ili kiongozi huyo ahamie na kwamba ikishakamilika atahudhuria sherehe ya uzinduzi.
Balozi huyo Rose Nzelemera anaishi katika nyumba ya kupanga jambo ambalo liliwafanya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kumchangia ili apate nyumba yake binafsi kwa sababu kiongozi wa shinda ndio mtu anaye anakipigania chama.
Chongolo yupo Iringa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuhamasisha uhai wa chama ngazi za mashina, pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi akiambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Sofia Mjema na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi Haji Gavu.