Ligi ya mabingwa barani Ulaya itaendelea  tena leo kwa michezo miwili ya mkondo wapili  hatua ya robo fainali, kuchezwa katika miji ya Leicester (England) na Madrid (Hispania).
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England, Leicester City watakuwa nyumbani King Power wakipambana kuweka rekodi ya kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza, pale watakapo wakaribisha Atletico Madrid kutoka Hispania.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Jumatano iliyopita huko Vincente Cardelon, Leicester City walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Atletico Madrid. Ili waweze kufuzu nusu fainali Leceister City wanahitaji kupata ushindi wa mabao 2-0 na kuendelea huku wapinzani wao Atletico Madrid wakihitaji kupata sare ya aina yoyote ile.
Gareth Bale
mchezo mwingine, Real Madrid wakiwa bila ya staa wao, Gareth Bale anayesumbuliwa na majeraha ya mguu watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu kuwaalika mabingwa wa Ujerumani, FC Bayern Munich ambao wametiwa chachu kwa urejeo wa mshambuliaji wao mahiri Robert Lewandowski aliyekosa mchezo wa mkondo wa kwanza kutokana na kuwa majeruhi.
Real Madrid wanaingia katika mchezo wa leo wakihitaji sare ama ushindi wowote, ili waweze kufuzu nusu fainali kwa msimu wa saba mfululizo.
FC Bayern Munich wao wataingia katika mchezo wa leo wakihitaji ushindi wa kuanzia mabao 2-0 na kuendelea.
Mara ya mwisho FC Bayern Munich kuifunga Real Madrid ilikuwa ni mwaka 2001, pale ilipoichapa kwa bao 1-0 lililofungwa na Mbrazil, Giovane Elber.

Video: Korea Kaskazini yasema iko tayari kwa vita na Marekani
Marekani yakanusha kuwaua wanamgambo 100 wa Al-Shabaab