Malinda mlango wa Azam FC Aishi Manula ameibuka na kuachia ujumbe mrefu ‘waraka’ kupitia account yake ya facebook baada ya jana kufungwa goli la aina yake dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Ujumbe wa Manula ambao aliuachia jana usiku mara baada ya game kumalizika unasomeka kama ifuatavyo;

Inasikitisha sana kuona soka la Tanzania linashindwa kuendelea mbele pia inauma sana kama watanzania tukiona nchi jirani zikisonga mbele kisoka kama Uganda na Rwanda angali Tanzania tumepata uhuru wetu mapema kabisa ila tunabaki kuona wenzetu wakisonga mbele nasi tukibaki pale pale kama sio kurudi nyuma. Binafsi nilikuwa najiuliza kwanini Tanzania tunawazechaji wazuri na kila tuendako inchi za wenzetu wanasifia wachezaji wa KITANZANIA kwamba ni timu nzuri .

Swali KWANINI HATUENDELEI KISOKA ANGALI TANZANIA KUNA WACHEZAJI WAZURI.

Jibu langu binafsi linaangukia upande wa waamuzi. Kiukweli waamuzi wa TANZANIA ni tofauti na waamuzi wa duniani kote, nashindwa kufahamu ni sheria gani ambazo waamuzi wa TANZANIA wanazitumia kuendeshea ligi yetu. Maana utumbo wanaoufanya viwanjani si wakawaida na sio mara chache imekuwa ni desturi yao.

Swali kwa CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU NCHINI.

Hivi ni kweli waamuzi huwa wanakizi vigezo na masharti mpaka mnawapa vyeti ikwa ajili ya kusimamia sheria 17 za mpira wa miguu?
Je, kabla ya kuanza ligi huwa mnawapeleka hospitali kwa ajili ya kucheki afya zao?.

Mfano: KUPIMA MACHO KAMA YANAUWEZO WA KUONA MBALI.
Maana ukija kwenye upande wa offside/mpira wa kuotea, yani huku ndo kunauozo mkubwa na hili ni janga kati ya majanga waliyonayo waamuzi wa Tanzania. Maana huwa najiuliza hivi kweli huwa wanaona au?  Yawezekana tukawa tunalaumu waamuzi wabovu kumbe wakawa hawaoni mbali.

MANENO YA WASHABIKI.

Washabiki huwa kelele zao kwa marefa wanapoonekana kuchezesha mpira bila kuzingatia sheria kelele zao ni kuwashutumu kuwa wamekula rushwa. Swali langu ni kweli yawezekana kila siku marefa wakawa wanakula rushwa.?

Jibu langu ni kwamba “sio kama wanakula rushwa ila ni kutojua kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu.
Pia je na kama hawajui kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu je wamepataje mamlaka ya kuchezesha soka letu?

Raisi wa TFF angalia jipu kubwa na ambalo limeiva na linasubiri kutumbuliwa tu. Na waamuzi ni kitu kikubwa sana ktk kuinua soka la nchi.

Ninamengi sana ya kusema kuzungumzia soka la nchi yetu na mtu yeyote anayetaka kuzungumzia mada hii anitafute nitamueleza kwa kina.

Nia na dhumuni la kuandika ujumbe huu ni tukio lililotokea uwanja wa Mkwakwani TANGA.
Coastal dhidi ya Azam FC.

Tukio ambalo golikipa wa Azam alipodaka mpira na kupatwa na maumivu makalio baada ya kujigonga chini na baada ya kupata maumivu yale ambayo yalimshindwa kuinuka na kutupa mpira nje na akanyosha mkono na kumuonyesha mwamuzi kuwa amepatwa na zoruba, chakushangaza ni mwamuzi kupuliza firimbi na kuonyesha faulo kuelekea lango la Azam.

Na kuna tukio kama hilo lilitokea uwanja wa Karume na mwamuzi alikuwa Nkongo kama sikosei baada ya kipa kupata zoruba na mpira akiwa nao na akaonyesha ishara kuwa kapatwa na maumivu basi mkongo alipuliza firimbi na kuwaita madokta, baada ya kumaliza kutibiwa kipa alichukua mpira na kuuachia chini akiashiria katoa fair kwa maumivu aliyopata kipa.

Sasa swali, mkongo alitumia sheria gani na huyu katumia sheria gan?

NIKO TAYARI KUZUNGUMZIA HILI MAHALI POPOTE NA MTU YEYOTE, KUHUSU NINI KIFANYIKE ILI SOKA LA TANZANIA LISONGE MBELE.

 

TFF Yasikitishwa Kupigwa Kwa Mwandishi
Picha: Diamond apata mapokezi ya kitemi Kenya