Wababe wa Sudan Al Hilal Omdurman, wamepanga kuweka Kambi DR Congo kabla ya kuikabili Young Africans katika mchezo wa Mkondo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/22.

Mchezo wa Mkondo wa Kwanza umepangwa kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumamosi (Oktoba 08), ambapo Young Africans itakuwa na nafasi ya kipekee ya kupambana nyumbani kabla ya kwenda ugenini Sudan kupapatuana na Al Hilal kati ya Oktoba 14-16.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Sudan, Kikosi cha Al Hilal kitafanya safari ya kuelekea Lubumbashi- Dr Congo, baada ya kucheza mchezo wa Kombe la Sudan (Sudan Cup), Siku ya Jumanne (Oktoba 04) dhidi ya Hilal Al-Fasher.

Jumatano (Oktoba 05), Kikosi cha Kocha Florent Ibenge kitaanza safari ya kwenda DR Congo kuweka kambi ya siku kadhaa kabla ya kuwasili Dar es salaam-Tanzania siku mbili kabla ya mchezo.

Itakapokua Kambini DR Congo, Al Hilal itacheza michezo ya Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya TP Mazembe na AS Vita Club ambazo pia zinashiriki Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Kocha Ibenge anaamini Michezo hiyo miwili itakisaidia kikosi chake kuwa na utayari wa kuja Tanzania kupambana na Young Africans ambayo inasifika kuwa na kikosi bora na imara kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Prof. Mkumbo: Hoja ziandaliwe mchakato wa marekebisho Sheria ya Habari
Kocha Mgunda: Sijapata mtu maalum safu ya ulinzi