Saa chache baada ya Bosi wa WCB, Diamond Platinumz kumualika Ali Kiba kuwa mmoja wa wasanii ambao angependa washiriki katika tamasha lake la Wasafi Festival, King Kiba amejibu kiaina.

Jana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo jijini Dar es Salaam, Diamond alisema kuwa tamasha hilo ni tamasha la kila mtanzania hivyo angependa wasanii wote wahusike, ikiwa ni pamoja na Ali Kiba.

“Wasafi Festival ni tamasha letu sote, tutajitahidi kuhakikisha kila msanii ambaye atakua tayari kushirikiana nasi, tutashirikiana naye. Tutafurahi sana endapo tukiwa na Ali Kiba ili kuonyesha muziki wa Tanzania ulivyo mkubwa,” alisema Diamond.

Hata hivyo, usiku wa kuamkia leo, Mfalme Kiba ambaye wengi wanasadiki kuwa ni hasimu wa kibiashara wa Diamond, ameweka post kwenye Twitter ambayo huenda ikawa ni jibu la kisanii kwa Diamond.

Alikiba ameweka picha ya utani ya mchekeshaji nguli, Mr. Bean na kuandika “Thank You for listening to my presentation’ (Asante kwa kusikiliza uwasilishaji wangu).”

Picha hiyo pia ameisindikiza na maneno “You are welcome (karibu) #Konki #mofayaalikiba #KingKiba.”

Ikumbukwe kuwa katika hotuba ya Diamond jana, alimtaja pia Konki Master Dudu Baya akimualika kushiriki tamasha hilo kwa maelezo kuwa anaamini mashabiki wake wamemmiss.

Ali Kiba na Diamond wamekuwa katika joto la kutoelewana tangu mwaka 2003/2004. Joto la tofauti zao lilikorezwa mwaka jana na ushindani wa ngoma zao mbili ‘Zilipendwa’ na Seduce Me zilizotoka ndani ya saa 24.

Deontay Wilder: Najisikia kama muuaji wa Fury
Wanafunzi 79 wa shule ya msingi watekwa

Comments

comments