Ali Kiba anaendelea kuwa gumzo nchini na nje ya mipaka ya nchi yetu kupitia wimbo wake ‘Seduce Me’ ambao umeendelea kuweka rekodi kubwa kwenye mtandao wa YouTube.

Saa chache zilizopita, ‘Seduce Me’ imeongeza namba kwa kuangaliwa zaidi ya mara milioni 2 kwenye mtandao wa YouTube ndani ya siku tatu, ikiendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa gumzo (trending) Tanzania na Kenya.

Hii ni rekodi ambayo haijawahi kuwekwa na msanii yeyote wa Afrika Mashariki kwa kipindi kifupi.

Katika hatua nyingine, Diamond Platinumz ametangaza kusikika Septemba Mosi kwenye wimbo mpya alioshirikishwa na mkali kutoka Nigeria, Pantoranking.

‘Simba’ ameeleza kupitia Instagram kuwa wimbo huo unaoitwa ‘Love You Die’ ni moto wa kuotea mbali.

“MY PEOPLE!!! MY NIGGA RANKING GOT SOMETHING DELICIOUS FOR YOU, COMING OUT THIS 1ST SEPT 2017

FT YOUR ONE AND ONLY, #LOVEYouDie,” ameandika akiambatanisha kipande cha video ya wimbo huo.

WCB inayomilikiwa na Diamond inaendelea kufanya vizuri na wimbo wake ‘Zilipendwa’ unaoshikilia nafasi ya pili kwa kuwa gumzo kwenye mtandao wa YouTube (trending), ukiwa umeangaliwa zaidi ya mara 1,300,000 ndani ya siku tatu.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 29, 2017
Video: Ofisi za IMMMA zililipuliwa na milipuko wa kienyeji- Polisi Dar