Sakata la picha za video za faragha za muigizaji Wema Sepetu pamoja na video za kiasherati au chafu za Amber Rutty limetajwa kuwa mtihani wa kisheria unaoweza kusababisha vifungo jela au faini ya mamilioni kwa wawili hao.

Hivi karibuni, video za Wema akiwa na mpenzi wake wakifanya yaliyopaswa kufanyika faragha (French kiss) zilichafua hali ya hewa ziliamsha makucha ya Mamlaka husika ikiwa ni pamoja na Bodi ya Filamu; lakini pia anasubiri hatua za Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Juliana Shonza.

Kwa upande mwingine, msichana aliyetajwa kwa jina la Amber Rutty, alimwaga upupu wa uchafu baada ya video inayomuonesha akifanya mapenzi kinyume na maumbile kuingia mtandaoni, na tayari yuko mikononi mwa polisi baada ya kujisalimisha.

Akizungumzia masakata hayo, mwanasheria Godfrey Lwasonga aliyeko jijini Dodoma ameeleza kuwa wawili hao wanaweza kushtakiwa kwa kukiuka kifungu cha 14 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015, ambayo inakataza mtu yeyote kwa kutumia kompyuta au kifaa kinachofanana na kompyuta kuchapisha au kusababisha kuchapishwa kwa picha za faragha (ponografia).

“Sheria hii ambayo ilitungwa mwaka 2015, ina vifungu vidogo vya kwanza, pili na tatu ambavyo vinakataza mtu yeyote asirushe picha za utupu yaani ponografia. Akikutwa na hatia anaweza kulipa faini isiyopungua milioni 20 au kifungo sio chini ya miaka 7 au vyote kwa pamoja kulingana na busara ya mahakama itakavyoona,” amesema Mwanasheria.

Hata hivyo, kwa upande wa Amber Rutty, yeye anakabiliwa na mtihani mzito dhidi ya Kanuni za Makosa (Pinal Code) namba 154, ambapo endapo atashtakiwa na kukutwa na hatia mahakamani anaweza kufungwa jela maisha au kifungo kisichopungua miaka 30 jela.

“Kwahiyo sasa ni jukumu lake yeye ambaye anatuhumiwa kusema ni kwanini sio yeye ambaye alirusha zile picha kwenye mitandao. Mtu anaweza kusema kwa urahisi tu kwamba mimi sijarusha hiyo picha kwenye mtandao, lakini kumbuka ukipoteza simu au kompyuta ni lazima kuwe na ripoti hiyo Polisi,” alisema.

“Sasa bila ripoti ya polisi ya kupotelewa sisi tunajuaje? Kama huenda ulimtumia mtu mwingine akarusha hizo picha au ni wewe ulirusha na sasa unaleta tu utetezi,” aliongeza.

Amber Rutty aliyekiri kurekodi video hizo chafu alidai kuwa simu ya mpenzi wake ilipotea na kwamba ‘mwizi’ ndiye aliyezirusha mtandaoni.

Kwa upande wa Wema ambaye tayari ameshapata adhabu ya kufungiwa na Bodi ya Filamu, aliomba radhi kwa video hizo kuonekana mtandaoni na aliomba asijitetee kwa lolole bali achukue lawama zote na kuahidi kuwa haitajirudia.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 30, 2018
Bahari hatarini kuwa na plastiki zaidi ya samaki, makampuni yajipanga

Comments

comments