Vyombo vya usalama nchini Marekani vinamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 22 kwa tuhuma za kumuua kwa risasi rapa maarufu, XXXTentacion.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Ofisi ya jeshi hilo ya Broward, anayeshikiliwa ni Dedrick Devonshay Williams wa eneo la Pompano Beach, Fla.

Imeelezwa kuwa kijana huyo amefunguliwa mashtaka ya mauaji pamoja na kupora gari. Pia, anashtakiwa kwa kuendesha gari bila kuwa na leseni inayoruhusiwa kisheria.

Idara ya jeshi hilo eneo la Florida imeeleza kuwa imebainika kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa kwenye kipindi cha matazamio/uangalizi (probation) hadi mwaka 2021, na kwamba aliingia kwenye probation kutokana na kukutwa na hatia ya wizi wa gari hapo awali.

“Ndani ya saa 48, #BSO  idara ya makosa ya jinai imemkamata Dedrick Devonshay Williams kwa kumuua Jahseh Onfroy, anayefahamika pia kama XXXTentacion. William alipelekwa mahabusu kabla ya saa moja usiku eneo la Pompano. Tutawapa taarifa zaidi,” inasomeka tweet ya wana usalama wa Broward, kwa tafsiri isiyo rasmi.

XXXTentacion

XXXTentacion aliuawa kwa kupigwa risasi Jumatatu katika tukio linalotajwa kuwa ni la ujambazi huko Broward, Florida. Rapa huyo aliyekuwa na umri wa miaka 20 alikuwa na gari lake kabla ya watu wawili kumshambulia kwa risasi.

 

Madereva watano wa Serikali wakamatwa kwa kuvunja sheria za barabarani
Video: Mfalme wa muziki Afrika Mashariki kujulikana, Wakali wa nchi tano…