Aliyekua kiungo wa Mashetani Wekundi (Manchester United) Ander Herrera, amefichua siri ya safari ya kuondoka klabuni hapo, kwa kusema hakupenda iwe hivyo kama ilivyochukuliwa na mashabiki wengi duniani.

Herrera ambaye kwa sasa anakipiga na mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain, amesema alitamani kuendelea kuitumikia Manchester United lakini mamwazo yake hayakuwa sawa na bodi ya uongozi ya Manchester United.

Amesema siku zote aliamini angedumu kwa mda mrefu klabuni hapo kutokana na mapenze ya dhati aliyokua nayo, lakini cha kushangaza aliingizwa kwenye orodha ya wachezaji waliouzwa mwishoni mwa msimu uliopita.

“Ninapotazama nyuma mwaka mmoja uliopita, nia yangu haikuwa kuondoka Manchester United. Nilikuwa na mawazo tofauti na bodi lakini ninawaheshimu. Na Nawaheshimu sana. Wao hufanya mambo kwa ajili ya timu “Manchester United” na sikubaliani na watu ambao wanasema hawafanyi kazi ipasavyo.”  

“Wanapambana sana ikiwa  mambo hayaendi sawa na wanajitahidi sana kuirudisha (kuiweka) Manchester United sehemu stahiki. Sikukubaliana na maamuzi mengine waliyofanya lakini hii hutokea katika mpira wa miguu. Hutokea katika kila kampuni.”

“Mbali na hayo, ninawaheshimu. Nilikuwa na uhusiano mkubwa na Ed Woodward na wamiliki walipokuja kwa hivyo sina chochote cha kuwalalamikia wao.

“Solskjaer, alinisaidia sana ili mimi nibaki, lakini mambo hayakuwa hivyo, walitokuja (United) baadae, na kwa wakati huo nilikuwa tayari nimefanya uamuzi wa kucheza huko Paris.” Alisema Ander Herrera alipohojiwa na ESPN.

Ander Herrera  On 4 Julai 04 – 2019, Herrera alisaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Paris Saint-Germain, akiwa kama mchezaji huru, na Septemba 14 alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa Ufaransa dhidi ya Strasbourg waliokubali kichapo cha bao moja kwa sifuri, akichukua nafasi ya Pablo Sarabia.

Rais Magufuli amkosha Laila Ali
Kabananga: Sijapokea tuzo yangu