Kiungo wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich Arturo Vidal atafanyiwa upasuaji wa goti, baada ya kupata majeraha akiwa mazoezini mapema hii leo.

Meneja wa FC Bayern Munich Jupp Heynckes amethibitisha kuumia kwa kiungo huyo kutoka nchini Chile.

“Alikua anajaribu kumzuia mwenzake kwa chini, lakini kwa bahati mbaya alipata maumivu makali sehemu za goti,” amesema Heynckes

“Nimezungumza na dokta. Na tayari ameshafanyiwa vipimo, majibu yanaonyesha ni lazima afanyiwe upasuaji. ”

Kwa taarifa hizo ni dhahir Vidal mwenye umri wa miaka 30, ataukosa mchezo wa nusu fainali wa kombe la Ujerumani dhidi ya Bayer Leverkusen utakaochezwa kesho, huku kukiwa na kila dalili za kuendelea kuwa nje ya kikosi cha The Bavarians katika kipindi cha msimu kilichosalia.

Mchezo mwingine muhimu ambao kiungo huyo ataukosa ni wa nusu fainali  ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid, utakaochezwa katikati ya juma lijalo.

Morocco kukaguliwa kwa fainali za dunia 2026
Wenyeviti PAC na LAAC wawakosoa Mawaziri kujibu hoja za CAG

Comments

comments