Meneja wa Msanii wa BongoFleva nchini Tanzania Aslay, Chambuso amesema kuwa mwanamuziki wake hataki kushindanishwa na mtu yeyote katika ufanyaji kazi zake na wala haimbi kwa kutegemea kupata sifa kutoka kwa watu wanaomtizama bali anaimba kwa faida yake.

Ameyasema hayo mara baada ya kutokea maneno siku za hivi karibuni kwa baadhi ya watu wakidai kuwa kasi ya Aslay kwenye utoaji nyimbo imepungua huku wengine wakisema hata kipaji chake kimeshuka kutokana na kutoa nyimbo ambazo haziwakongi nyoyo mashabiki.

“Tunachokifanya sio kibaya ni kizuri kwa sababu sio kila nyimbo ya Aslay utaipenda nyingine utaiona kawaida, tumekupa ngoma mbili chagua moja utakayoona wewe inakufaa. Kwa hiyo mtu akiona kasi ya Aslay imepungua au kutaka na kumfananisha na mtu fulani atakosea, kwa sababu Aslay anafanya muziki wake yeye kama yeye na hataki kushindanishwa na yeyote na wala hafanyi kwa kutaka sifa kwa watu,”amesema Chambuso

TLS waonywa, watakiwa kuacha uanaharakati
Video: Tishio la Mange lawaibua Marekani na Uingereza, ATCL yawasha moto bungeni

Comments

comments