Diamond Platinumz ameangusha moto kwenye paa la Bongo Flava na wimbo wake mpya ‘Fire’ na kumuweka ndani mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu na mama watoto wake, Zari.

Simba Dangote ambaye hivi karibuni aliweka wazi kuwa yuko karibu sana na Tanzania Sweetheart ‘Wema’, ameonesha kuendelea kulikubali umbo la mrembo huyo huku akiuweka karibu uzuri wa sura ya Zari.

Katika ngomba hiyo mpya aliyomshirikisha Tiwa Savage ambaye ni mwanafamilia wa lebo ya Roc Nation ya Jay Z, Mondi amemuelezea mpenzi wake anayemuimba akimfananisha na warembo hao wawili kwa jinsi alivyoumbika.

Nyuma kama sunami, Sura Zarina Zari… shape Sepetu Wema,” anasikika Diamond kwenye wimbo huo ambao video yake inaweza kuachiwa rasmi muda wowote.

‘Fire’ umepikwa ndani ya studio za Wasafi na mkono wa mpishi wa hits za WCB, Lizer umehusika.

Bofya HAPA kuupakua Fire.

Video: CUF wamaliza mgogoro wao, wapata bodi mpya inayotambuliwa na msajili
JPM azindua Viwanda vitatu mkoani Pwani