Kiungo wa klabu ya Arsenal Granit Xhaka amesema almanusura alikua akose nafasi ya kuendelea kuwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uswiz, kufuatia jeraha la mguu, alilolipata akiwa katika mazoezi.

Xhaka alipatwa na majeraha ya goti la mguu wake wa kushoto, baada ya kuteleza uwanjani, kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo la mji wa Lugano, Uswiz ilipoweka kambi timu ya taifa ya nchi hiyo, ikijiandaa na fainali za kombe la dunia.

Shirikisho la soka nchini Uswiz limeripoti kutokea kwa tukio hilo, lakini limethibitisha Xhaka kuwa salama, baada ya kufanyiwa vipimo vya MRI, na kuonekana hakupatwa na majeraha makubwa kama ilivyodhaniwa awali.

“Ninaendelea vizuri.” alisema Xhaka kupitia tovuti ya shirikisho la soka nchini Uswiz.

Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, atakosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki siku ya jumapili dhidi ya Hispania, lakini anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 23 kitakachokwenda urusi kupambana.

Kwa sasa Xhaka ni sehemu ya kikosi cha Uswiz chenye wachezaji 26 walioitwa na kocha Vladimir Petkovic 26, sambamba na kiungo wa Stoke City Xherdan Shaqiri na Stephan Lichtsteiner anaewaniwana Arsenal.

Timu ya taifa ya Uswiz itaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa dunia, kwa kucheza dhidi ya Brazil Juni 17, kabla ya kukutana na Serbia na baadae Costa Rica katika michezo ya kundi E.

Video: Tazama Diamond akifunga ndoa na Zari ndani ya 'Iyena'
Waziri wa Elimu avurugwa na Kwaya ya Utupu ya Wanafunzi