Msanii wa muziki wa Bongofleva nchini, Ben Pol amesema kuwa kuna kazi anafanya na mtayarishaji wa muziki mkubwa wa Marekani ambaye amefanya kazi na wasanii kama Busta Rhymes, Jennifer Lopez, Trey Songz na wengine.

Ben Pol amesema tayari ametumiwa beat na ameanza kuifanyia kazi, ingawa amesema hawezi kumtaja mtayarishaji huyo kwani ni mapema.

“Kuna kazi nafanya na producer mkubwa wa Marekani ila siwezi kumtaja, kwani ni mapema sana lakini tayari ameshafanya kazi na wasanii kama Busta Rhymes, Jennifer Lopez, Trey Songz na wengine na hivi sasa ameshanitumia beat na nimeanza kuifanyia kazi,” alisema Ben pol.

Ben Pol amesema kwa sasa mipango hiyo imefikia katika hatua nzuri na mtayarishaji huyo ambaye ameeleza kuwa amekutana naye baada ya ‘ku-like’ picha zake katika ukurasa wa Instagram.

“Kuna siku jamaa ‘ali-like’ picha zangu Instagram. Baada ya kuona hivyo nami nikaanza kumfuatilia, na ndipo nilivyokuja kujua kua ni mtu mkubwa sana.

Amesema baada ya hapo alianza kuwasiliana naye, akamtumia baadhi ya kazi zake, “kuna vitu akawa ananishauri kuhusu muziki, na ninamshukuru Mungu kwamba kila kitu kwa sasa kinaenda vizuri,”

Ben Pol amewataka mashabiki wake wajue kwamba kuna mambo mengi makubwa yanakuja siku za usoni.

Tanzia: Baba mzazi wa msanii Belle 9 afariki dunia
Jose Mourinho Kurusha Ndoano Borussia Dortmund