Nyota wa muziki wa pop na mbunge wa upinzani nchini Uganda ‘Bobi Wine’ amefanya tamasha lake kwanza tangu ashtakiwe na kufungwa kwa mshtaka ya uhaini.

Katika tamasha hilo la Bobi Wine kulikuwa na idadi kubwa ya polisi, ambapo liliruhusiwa tu kufanyika kwa sababu halikuwa la kisiasa.

Aidha, Bobi Wine anadaiwa kuteswa na kupigwa akiwa kizuizini mwezi Agosti mwaka huu, madai ambayo yalikanushwa na mamlaka.

Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kuwa changamoto kubwa kwa rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

Baadhi ya maelfu ya watu waliohudhuria katika tamasha hilo walikuwa wamevalia nguo nyekundu, rangi inayohusishwa na vuguvugu la Bobi Wine la People Power.

“Ninashukuru polisi wa Uganda kwa kutupa ulinzi mkubwa kwa ajili ya usalama wetu, lakini sio kama hapo awali walipokuwa wakituzuia,”amesema Bobi Wine

 

Agoma kutoka jela, adai anafundisha wafungwa kutumia Facebook
Picha: Polisi waonesha nyumba aliyofichwa Mo Dewji alipotekwa

Comments

comments