Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limejadili hatima ya mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kuhusu malipo ya mshahara wake.

Mjadala huo umeibuka mara baada ya Mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ CCM, kuhoji ni lini Bunge litasitisha mshahara wa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Aidha, akijibu hoja hiyo, Ndugai amesema kuwa kuna haja ya kulitazama jambo hilo kwa upekee kwani Mbunge huyo wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa sasa hayupo Bungeni, hayupo Tanzania, hayupo Jimboni kwake, hayupo hospitalini kama ambavyo taarifa zinavyosomeka kuwa ni mgonjwa na pia hakuna taarifa yeyote ya daktari inayoelezea kuwa ni mgonjwa.

“Tulikuwa tunajua yupo hospitalini sasa tunaambiwa yupo duniani, kwa maneno ya Msukuma anadhurula, kwahiyo nikuhakikikshie mheshimiwa msukuma yale yaliyo ndani ya uwezo wangu nitayafanya,” amesema Ndugai.

Lissu kwasasa yupo ziara barani Ulaya pamoja na nchi za Amerika ya Kaskazini ambapo ameonekana akifanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari kuzungumzia shambulio lake.

 

 

 

Masilingi, Lissu ngoma mbichi, 'Ni bora urudi Tanzania ukasaidie upelelezi'
Kesi ya Mauaji Mwanafunzi Spelius yasikilizwa kwa mara ya kwanza