Bondia wa Mexico, aliyekuwa bingwa wa masumbwi wa dunia uzito wa middleweight, Saul ‘Canelo’ Alvarez amefungiwa kushiriki mchezo huo kwa kipindi cha miezi sita baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya vipimo vya matumizi ya dawa zisizostahili.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamisheni ya Michezo ya Nevada (Nevada State Athletic Commission).

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 27 amelazimika pia kuahirisha pambano la marudiano kati yake na Gennady Golovkin lililokuwa limevuta mashabiki wengi zaidi mwaka huu.

Canelo na timu yake wamejitetea kuwa hakutumia dawa zozote zilizokataliwa bali nyama alizokula zilikuwa zimehifadhiwa kwa kemikali ambazo zimeleta matokeo hayo. Wamesema kuwa nyama hizo zimewaathiri wachezaji wengi wa nchi hiyo.

Hata hivyo, tarehe ya kuanza adhabu yake imerudishwa nyuma kutokana na kusimama kujihusisha na mapambano tangu alipotuhumiwa, hivyo atakuwa huru kuanzia Agosti 17 mwaka huu.

Kampuni inayosimamia kazi zake ‘Golden Boy Promotions’ iliyo chini ya Oscar Delahoya imesema kuwa mpambanaji huyo atarejea uringoni Septemba mwaka huu, wikendi ambayo Mexico itakuwa ikiadhimisha siku yake.

Picha: Alikiba afunga ndoa na binti wa Mombasa
Picha: Kikwete apewa tuzo Marekani