Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza njia mpya ya kuitekeleza kampeni yake ya UKUTA baada ya kuahirisha mara mbili maandamano na mikutano nchi nzima.

Jana, Chadema kwa mara ya pili walitangaza kuahirisha maandamano na mikutano nchi nzima waliyotangaza kuifanya leo na badala yake wametangaza njia mpya watakayoitumia kufanikisha kampneni yao wanayodai ni ya kupambana na udikteta nchini.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema kuwa wamebaini fikra ya UKUTA inapaswa kupandikizwa kwa muda mrefu kwa wananchi ili waielewe vizuri na kwamba hawataitangaza tarehe mpya kwa kuhofia vyombo vya usalama kujipanga kuwadhuru wafuasi wao.

Akitangaza mbinu mpya watakayoitumia, Mbowe alisema kuwa kwanza wamejipanga kufungua kesi mahakamani kupinga agizo la kuzuiwa mikutano na maandamano ambayo amedai ni haki ya kikatiba ya vyama vya kisiasa nchini.

Aidha, alisema viongozi wa chama hicho wataanza kuvuka anga la Tanzania na kufikisha malalamiko yao kwenye nchi marafiki wa nchi yetu kuhusu hali ya kisiasa nchini.

Alisema kuwa tayari ziara ya kwanza iliyofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji  na kamati ya chama hicho nchini Denmark na Ujerumani imeonesha matunda na kwamba watazulu pia nchi nyingine zikiwemo Ujerumani na Uingereza.

Aidha, Mbowe alisema kuwa ndani ya nchi, wataendelea kuzungukia matawi yote ya chama hicho na kufanya vikao vya ndani kwa lengo la kuimarisha chama na kuendeleza harakati za UKUTA.

“Kufuatia kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya vyama vya siasa, tutafanya ziara katika Kanda na Mikoa ya kichama ili kuendeleza harakati za Ukuta na kujenga uhai wa Chama na Ukawa,” Mbowe anakaririwa.

Katika hatua nyingine, wakati Chadema wakizungumzia kupambana na udikteta nchini, Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza wiki hii ilitoa matokeo ya utafiti wake unaoonesha kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanasema hakuna udikteta nchini.

Diamond athibitisha bifu na King Kiba sasa bhaasi.
PPRA yanusa harufu ya rushwa TCRA, Ofisi ya Bunge, Wizara ya Maji…