Bondia Francis Cheka amelitaka Taifa pamoja na Rais John Magufuli kujivunia ushindi aliouleta nyumbani Jumamosi iliyopita baada ya kumpiga bondia mbabe na raia wa Serbia, Gerard Ajetovic.

Kupitia ushindi huo, Cheka alifanikiwa kutwaa taji la WBF akimpokonya mpinzani wake huyo ambaye alieleza kutoyaamini matokeo.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Cheka alisema kuwa ataendelea kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha anazidi kuliletea Taifa heshima hadi kuchukua ubingwa wa dunia, huku akimuomba Rais John Magufuli pia kujivunia ushindi huo.

‘Magufuli akiuona ushindi huu, ukiwa ni ushindi wa kwanza tangu aingie madarakani katika siku zake zaidi ya mia moja na tano hivi. Kwa sababu tangu aingie ni mimi na Mbwana Samatha tumeleta ushindi mkubwa nyumbani,” alisema.

Francis Cheka na Mdogo wake ambao wote walipata ushindi Jumamosi katika mapambano tofauti, leo wametoa shukurani kwa watanzania na kuahidi kuendelea kusaka ubingwa zaidi.

 

Polisi wapekua Nyumba ya Halima Mdee, watoka na hili
Kiwanda cha Vipodozi Feki chanaswa Kigamboni Dar