Klabu ya Chelsea huenda ikafanikiwa kumsajili kwa urahisi, mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya Olympique Marseille, Michy Batshuayi, kutokana na mgomo wa wazi wazi aliouonyesha wa kukataa kujiunga na West Ham Utd.

Batshuayi alikua ameshawekwa katika mpango wa kuuzwa katika klabu ya West Ham Utd, lakini amepingana na viongozi wake kwa kuweka msisitizo wa kutaka kucheza katika klabu yenye ushindani katika ligi ya nchini England.

Chelsea wameripotiwa kutenga kiasi cha Pauni milioni 31kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, kwa kigezo cha kuamini Stamford bridge patakua mahala sahihi kucheza soka lake la ushindani.

The Blues wametajwa kuingia katika mbio za kumsajili Michy Batshuayi, baada ya kuona huenda kukawa na ugumu wa kumrejesha aliyewahi kuwa mshambuliaji wao Romelu Lukaku ambaye napigiwa upatu wa kujiunga na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC akitokea Everton.

Brazil Yakumbuka Kichapo Cha Kufungwa Mabao Saba
Liverpool, West Ham United Zamuwania Thomas Vermaelen