Chris Brown amemvaa rapa Offset akimtaka ajitokeze wapigane baada ya kupishana kauli kuhusu sakata la rapa 21 Savage kutimuliwa nchini Marekani alipobainika kuwa sio raia wa nchi hiyo na hakuwa na vibali husika.

Ugomvi kati ya wasanii hao uliibuka baada ya Chris Brown kuweka kwenye mitandao ya kijamii ‘meme’ ya kumkejeli 21 Savage, na ndipo Offset aliamua kumvaa akimkosoa kuwa ‘hazichekeshi’.

Offset ambaye ni rafiki wa karibu wa 21 Savage, alionesha kuchukizwa zaidi na Chris Brown na kuhamia Twitter ambako alifunguka zaidi akimshambulia kwa kumkejeli rafiki yake aliyekumbwa na matatizo.

Hata hivyo, Breezy alienda mbali akimwaga matusi kumjibu Offset, akimtaka kuachana na kuandika kwenye mitandao ya kijamii na badala yake wakutane wapigane kama wanaume wababe. Matusi hayo tumeyaweka kando kwa sababu za kimaadili.

Hata hivyo, baadaye Breezy aliifuta picha yenye maelezo hayo kwenye sura ya kawaida ya Instagram na kuhamia kwenye Instagram Stories ambako aliendeleza mashambulizi yenye matusi mazito.

Chris Brown na Offset wamekuwa maadui kwa muda, hasa baada ya kuwepo tetesi kuwa mwimbaji huyo anataka kumnyemelea mama mtoto wa Offset, Cardi B baada ya taarifa kuwa wameachana.

Marekani yatahadharisha mpango wa shambulizi lingine Kenya
Mwanafunzi darasa la kwanza abakwa, apewa ujauzito

Comments

comments