Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United Marouane Fellaini amethibitisha kufanyiwa vipimo na kukutwa na virusi vya Corona.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Shandong Luneng ya China, ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter “Nitarejea kwenye majukumu ya soka hivi karibuni “.

Baadhi ya vyombo vya habari vya China vimeripoti kuwa Fellaini, ametangwa kwenye hospitali ya Jinan, ambayo ni maalum kwa ajili ya wagonjwa wa virusi vya Corona.

Taarifa ya klabu ya Shandong Luneng imeeleza kuwa: “Ni dhahiri amefanyiwa vipimo na amebainika kuwa na virusi vya Corona, kwa sasa amewekwa KARANTINI, na anaendelea vizuri”.

Fellaini, alirejea nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuendelea na mazoezi binafsi kufuatia kusimamishwa kwa ligi ya China, amesema ahisi maumivu yoyote, zaidi ya kuheshimu taratibu wa kujitenga ili kuepuka kuwaambukiza wengine.

Kiungo huyo kutoka nchini Ubelgiji, alijiunga na klabu ya Shandong Luneng mwaka 2019, akitokea England alipocheza soka kwa muda wa miaka 11 akiwa na klabu za Machester United na Everton.

Tanzia: Watumishi watano TRC wafariki kwa ajali
Rais wa Botswana awekwa karantini siku 14

Comments

comments