Aliyewahi kuwa meneja wa klabu za Liverpool, Newcastle United na Real Madrid Rafael Benitez ameachia ngazi kama Kocha Mkuu wa Klabu ya Dalian Professional inayoshiriki Ligi ya China (Chinese Super League), kwa makubaliano na viongozi wa klabu hiyo.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania alikuwa amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja, huku akilipwa mshahara wa Pauni milioni 12 kwa mwaka, ambapo alianza kufanya kazi Julai 2019, muda mfupi baada ya kuondoka Newcastle United.

Benitez mwenye umri wa miaka 60, amesema amefanya uamuzi huo kwa sababu ya wasiwasi juu ya afya na ustawi wa familia yake wakati wa janga la Corona.

Hata hivyo habari hizi huenda zitawavutia sana mashabiki wa Newcastle United, ambao wanamkubali Benitez kufuatia mafanikio ya miaka mitatu huko St James ‘Park kati ya 2016 na 2019.

Mashabiki wa Newcastle United wamechishwa na meneja wao wa sasa Steve Bruce kutokana na mambo kuwaendela kombo kwenye michezo ya Ligi Kuu huku wakwa wameshatolewa kwenye michuano ya kombe la FA.

Benitez ni miongoni mwa mameneja wanaopendekezwa kuchukua nafasi  yay a Bruce endapo The Magpies wataamua kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi katika kipindi hiki.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 26, 2021
Ozil: Sitaisahau Arsenal, ninaipenda na kuithamini