Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Joketi Mwegelo ambaye pia ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama amewataka vijana vijana wanaopatiwa mafunzo ya mgambo kuhakikisha wanadumisha uzalendo na kuwa walinzi wa amani.

Mwegelo ametoa agizo hilo wakati akifungua mafunzo yamiezi minne kwa vijana hao ambao miongoni mwao wanawake ni 62 na wanaume ni 68 wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 25.

Aidha amesema vijana wanaopatiwa mafunzo hayo wanatakiwa kutokubali kurubuniwa na wenye nia za kuvuruga amani ya nchi.

Pia amewataka kuweka kipaumbele katika kulinda amani na utulivu hasa wakati Taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu

Hata hivyo Mkuu wa wilaya hiyo ameagiza wasichana waliopo katika mafunzo hayo wanapatiwa taulo za kike ili kuongeza moyo wakiwa mafunzoni.

Gavana wa Benki Kuu aipongeza PPRA
Lebanon: waandamana kutaka viongozi wajiuzulu