Saa chache baada ya kumalizika kwa tuzo za MTV MAMA ambazo wasanii wa Tanzania walitoka kapa, Tanzania ilitajwa mara nne jukwaani kunyakua tuzo za African Entertainment Awards USA (AEA – USA) zilizotolewa New jersey, Marekani.

Diamond alitajwa kuwa mshindi wa tuzo ya Best Male Single na Best Collaboration (Wimbo bora wa Kushirikiana) akiungana na AY kwa ‘Zigo Remix’.

D-J D Ommy wa Clouds Fm ameendelea kuweka historia ya kuwa mchezea santuri pekee Afrika Mwenye tuzo, baada ya kutajwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezea santuri bora zaidi Afrika (Best Dj in Africa). Hii ni tuzo ya pili ya kimataifa kwa DJ-D Ommy ambaye wiki chache zilizopita alishinda tuzo ya AFRIMMA katika kipengele kama hicho.

dj-d-ommy

Harmonize alifanikiwa kubeba tuzo ya Msanii bora Mpya (Best New Artist) na kuongeza tuzo nyingine kwa lebel yake ya WCB.

Tuzo hizo zilirushwa mubashara na kituo cha runinga cha Trace Urban.

Real Madrid Yazipiga Kumbo Sevilla CF, FC Barcelona
Ndalichako, Mahiga wawavuruga Chadema, CCM wajichagulia Meya bila mpinzani