Klabu ya Azam FC umemtambulisha rasmi mshambuliaji Donald Dombo Ngoma kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo katika msimu ujao wa 2018/2019.

Mzimbabwe huyo mwenye umri wa miaka 28 ametemwa na klabu ya Yanga kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu na sasa anakwenda kujiunga na wana ramba ramba katika dimba la Chamazi.

Ngoma alijiunga na Young Africans mwaka 2015 akitokea FC Platinums ya nyumbani kwao Zimbabwe.

Yanga wameshindwa kutetea ubigwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu na mpaka sasa wako katika nafasi ya tatu huku Azam FC ikishika nafasi ya pili.

 

Polisi wamvua nguo mwanamke wakidai wanafanya uhakiki
Zaidi ya watu 100,000 huumwa na nyoka, WHO yapitisha azimio