Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa ya Ulaya (EMA), imeonya kuwa baadhi ya chanjo za Uviko-19 zinaweza kusababisha akina mama kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi.

EMA kupitia Wataalamu wake, imetaka ugunduzi huo uongezwe katika orodha ya uwezekano wa athari inayoweza kutokea huku ikitaja chanzo za Pfizer na Moderna, kuonesha athari hizo na hasa katika chanjo ya pili au zaidi.

Taarifa ya mamlaka hiyo, imesema hali hiyo imebainika katika uchunguzi wa kitabibu ambapo hedhi huongeza kiwango cha utokaji damu au kutoka kwa muda mrefu na kuathiri ustawi wa afya kutokana na chanjo hiyo.

Chanjo ya Uviko-19.

Hata hivyo, Msemaji wa Moderna amesema kampuni yake ina taarifa za ripoti ambazo zinahusisha chanjio ya “dysmenorrhea” kuleta maumivu wakati wa kipindi cha hedhi, ingawa bado hawajagundua athari zenye kuhusiana na chanjo ya Moderna, Spikevax. 

Kampuni ya BioNTech yenye kutengeneza chanjo ya Pfizer haikuweza kupatikana mara moja kueleza kuhusu ripoti hiyo huku EMA ikisema ripoti ya uchunguzi wake haina ushahidi wa wazi unaonesha matatizo ya hedhi yanayowapata baadhi ya kina mama yana athari yoyote katika suala la afya ya uzazi na uzazi wao.

Matukio ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, yamekuwa yakifanyiwa uchunguzi katika ngazi ya Kimataifa hasa katika bara la tangu ripoti za kwanza kuonekana kwa wanawake waliochanjwa.

Jamii yahimizwa ustawishaji wa mazingira
Mashindano ya 12 duniani urembo,utanashati kwa viziwi kufanyika Tanzania