Mshambuliaji wa Man City Sergio Aguero, amefunguliwa mashtaka na chama cha soka nchini England (FA) kwa tuhuma za kuonyesha mchezo usio wa kiungwana wakati wa mpambano wa ligi kuu ya soka nchini humo (PL) dhidi ya West Ham.

Picha za marudio za televisheni zilimuonyesha Aguero, akimpiga kiwiko beki wa West Ham Utd Winston Reid katika mpambano huo, ambao ulinguruma mwishoni mwa juma lililopita, hatua ambyo iliibua mijadala mbalimbali miongoni wa wadau wa soka.

Chama cha soka nchini England (FA), kimempa muda Aguero mpaka jioni ya hii leo, ili awasilishe utetezi wa kupinga tuhuma zinazomkabili kabla ya kamati ya nidhamu haijakutana na kuendelea na masuala mengine ya hukumu.

Endapo mshambuliaji huyo atashindwa kuwasilisha utetezi utakaoishawishi kamati hiyo, atafungiwa michezo mitatu iliyo chini ya chama cha soka nchini England (FA), ambapo adhabu hiyo itaanzia katika mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Man Utd ambao umepangwa kuchezwa Septemba 10.

Michezo mingine ambayo ataiokosa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, kama atakutwa na hatia ni dhidi ya Bournemouth (ligi kuu) pamoja na mchezo wa kombe la ligi (EFL) dhidi ya Swansea City.

Christian Benteke Afunguka, Asema Klopp Alishindwa Kumuelewa
Ajitolea kukatwa kichwa kipandikizwe kwa mtu mwingine kwa majaribio