Afya ya kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson imeimarika na ameruhusiwa kutoka Hospitali na kurudi nyumbani kuendelea na matibabu ya kawaida.

Wiki tatu zilizopita Ferguson alilazwa katika Hospitali ya Salford Royal baada ya kufanyiwa upasuaji wa ubongo.

Gazeti la ‘The Sun’ limeripoti kuwa Ferguson mwenye umri wa miaka 76 anaelendelea vizuri na anategemea kurudi Old Traford katika bodi ya Wakurugenzi.

Kabla yakustaafu mwaka 2013 Sir Alex Furguson amewahi kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu Soka nchini Uingereza katika kipindicha miaka 26 alipokuwa akiifundisha Manchester United.

 

 

Rais Magufuli apandisha cheo maafisa 9 magereza
JPM azidi kuwapa mashavu Majaji