Kocha Mkuu Mpya wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin alikuwa sehemu ya mashuhuda wa mchezo wa Taifa Stars dhidi ya DR Congo.

Taifa Stars ilicheza nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam leo Jumatano (Novemba 11) na kupoteza mchezo huo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 kwa kufungwa mabao 3-0.

Kocha Franco ambaye aliwasili Jijini Dar es salaam jana Jumatano (Novemba 10), aliahidi kwenda Uwanja wa Mkapa na amefanya hivyo.

Hata hivyo huenda Kocha huyo kutoka nchini Hispania akawa amepata kuwatambua vizuri wachezaji wa Simba SC ambao walikuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kichocheza dhidi ya DR Congo.

Tayari Kocha Franco alishawaona wachezaji wa Simba SC waliobaki kambini na alipata wasaa na kuzungumza nao kwa uchache, baada ya kufika kambini hapo Jana Jumatano.

Simba SC ambayo ni Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea na Mshike Mshike wa Ligi hiyo Ijumaa (Novemba 19) kwa kuvaana na Ruvu Shooting.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 12, 2021
Mbowe na wenzake washinda pingamizi