Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amesema kuwa amejipanga kumaliza migogoro yote ya ardhi na mivutano ya kimipaka ya kiutawala kati ya Wilaya moja na nyingine ndani ya miaka miwili.

Ameyasema hayo katika kikao cha ardhi,kilimo,mifugo na mazingira kilichowakutanisha wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi,Wenyeviti wa Halmashauri pamoja na maofisa wengine kujadili kwa kina mbinu za kumaliza migogoro hiyo.

Gambo amesema kuwa baada ya uhakiki wa mipaka na ushuri kutolewa katika eneo husika,mtu atakae bainika kuhusika na uvunjifu wa amani atachukuliwa hatua kali.

“Tunataka  sasa tuachane na migogoro ya ardhi na mipaka, ninawaagiza wataalamu wa ardhi kulifanyia kazi hili suala katika kipindi tulichopeana baada ya hapo hatutakuwa na huruma kwa wanajitafutia umaarufu kupitia migogoro ya ardhi

Rais mstaafu wa Ureno, Mario Soares afariki dunia
Chadema yatoa siku saba kwa DC kurejesha misaada yao