Klabu ya Watford imemtangaza, Javi Gracia kuwa kocha mpya wa timu hiyo baada ya kumtimua kocha aliyekuwa akiifundisha Klabu hiyo, Marco Silva.

Kocha huyo mpya raia wa Hispania amesaini mkataba wa miezi 18 ikiwa ni kibarua chake kingine tangu aachane na kazi ya kuinoa klabu ya Rubin Kazan mwezi June mwaka jana,

Aidha, Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 amefundisha vilabu vya Ligi mbalimbali katika nchi za Hispania na Ugiriki.

Hata hivyo, Gracia anakuwa kocha wa 10 kufanya kazi ya kukinoa kikosi hicho cha Watford chini ya familia ya Pozzo tangu mwaka 2012.

Hukumu ya Sugu kujulikana leo
Gwajima atangaza mazishi ya mama yake