Malinda mlango kutoka nchini England, Joe Hart anajiandaa kuondoka Etihad Stadium baada ya kuendelea kuona dalili za kutokua sehemu ya mipango ya meneja wa sasa wa Manchester City, pep Guardiola.

Tovuti ya Skysports imeeleza kuwa, mlinda mlango huyo amekua hana furaha tangu mwishoni mwa juma lililopita, baada ya kuachwa katika kikosi cha kwanza ambacho kilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Sunderland, kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England.

Guardiola ameonyesha kutomuhitaji Hart kwa sasa, baada ya kuendelea kuhusishwa na taarifa za kutaka kumsajili mlinda mlango wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona Claudio Bravo, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa zilizoripotiwa na kituo cha Skysports na kuandikwa katika tovuti ya televisheni hiyo ya England zinaeleza kuwa tayari uongozi wa Man City umeshakubali kutoa kiasi cha pesa ambacho kimeombwa na FC Barcelona kama ada ya usajili wa mlinda mlango huyo kutoka nchini Chile.

Hata hivyo Guardiola amediriki kuzungumzia mustakabli wa Hart alipokua katika mkutano na waandishi wa habari mjini Bucharest nchini Romania na kuonyesha uhakika wa kuwa tayari kumuacha aondoke.

“Tunajua Joe Hart anajiandaa kufanya maamuzi ya mustakabali wake, na jibu litapatikana siku chache zijazo.”

“Kuna taarifa zinazomuhusu na nimesikia klabu kama Sevilla ya Hispania pamoja na nyingine kutoka England zimeonyesha nia ya kumsajili, hivyo tunasubiri kuona kama watawasilisha ofa nzuri kwa ajili yake.” Alisemna Guardiola wakati wa mkutano na waandishi wa habari kabla.

Klabu ya Everton ya nchini England inapewa nafasi kubwa kumsajili Joe Hart kutokana na mchezaji huyo kuonyesha dhamira ya kutaka kuendelea kubaki kwenye mzingira ya nyumbani kwao.

Hart mwenye umri wa miaka 29 alisajiliwa na Man City mwaka 2006 akitokea kwenye klabu ya mji wa nyumbani kwao Shrewsbury. Na kwa kipindi chote alichokaa Etihad Stadium amefabnikiwa kucheza michezo 347 na amefungwa mabao 347.

Cesc Fabregas Awachunia Mashabiki Wake
Video: TRA imeuleta mfumo kuhakiki, kuboresha taarifa za mlipa kodi